https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEje_9NoQUALZgiCr1ZoP3CqzN1Xlp8k6oGfsxR3DZAP-eBrY47OeJcocbdrMikPRFFBL9E_LcJszXiVFPdSSsSlLec_FONyumC-ACLsgnImcvPf_XOIv07Oiqse1lg4AeQgaM4Fm4FEV9k/s1600/ginger-powder-benefits.jpg

TANGAWIZI NI NINI?
Tangawizi nikiungo ambacho kinatokana na mmea wa Tangawizi ambao unafanana sana na mmea wa binzari, mathalani Binzari humenywa maganda na kusagwa kwa ajiri ya matumizi lakini tangawizi hubakia kama mzizi na hupatikana maeneo mbali mbali kama sokoni, mtaani, ikiuzwa.

Tangawizi hupatikana Nchi nzima na kwa bei nafuuu ambayo kila mtu anaweza kuimudu, Hupatikana kwa kipande, fungu, ama kilo ama debe na huuzwa na kununuliwa na watu wa aina zote na rika zote na wenye uwezo wowote kiuchumi

FAIDA NA UMUHIMU WA TANGAWIZI MWILINI.


  • Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wanawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.
  • Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.
  • Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
  • Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.
  • Husaidi kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.
  • Tangawizi husaidia kupunguza maumivu mwilini.
  • Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu.
  • Husaidi kuponya fluu kwani chai ya tangawizi ni salama
  • Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya
    usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula.
  • Matatizo ya Moyo: Tangawizi huimarisha moyo wa binadamu na kumwepushia maradhi ya moyo. Hii ni kwa kuwa inapunguza kiwango cha mafuta mwilini.
  • Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.
  • Huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na shinikizo la mawazo, kisunzi, na kukosa umakini.