Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo
kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida
zake mwilini.
Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama
mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano
na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake.
Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China.
Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya
na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania.
FAIDA ZA BIZARI KIAFYA
Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha
katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi
unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako.
Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga
ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha
kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuzuia mtu kuzeeka kabla ya wakati.
Aidha, bizari huimarisha sehemu za magoti hivyo kukuepusha na matatizo
ya miguu kuuma. Bizari pia hun’garisha ngozi na kuifanya kuwa yenye afya
na huimarisha pia mfumo wa usagaji chakula (Digestion).
SUALA LA UBORA NI MUHIMU
Katika ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolijia tulionao sasa,
bizari hutengenezwa viwandani na kuhifadhiwa kwa usafirishaji sehemu
mbalimbali duniani na kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu. Katika hali
kama hiyo, si ajabu kukuta bizari iliyoongezewa kemikali zingine za
kuhifahdia chakula.
Bizari ya aina hiyo, tayari inakosa faida zilizoelezwa hapo juu, hivyo
ni suala muhimu kuangalia ubora wa bizari unayoitumia na mahali
inapotoka. Katika nchi yetu, Mungu ametujaalia ardhi yenye rutuba ambapo
kiungo kama hiki kinalimwa na kupatikana kwa wingi na kwa uhalisia
wake.
Katika suala la kujali ubora, pendelea zaidi kununua bizari kutoka
sokoni ambayo imetengenezwa katika mazingira safi na salama na bila
kuchanganywa na kitu kingine. Iwapo pia utanunua bizari iliyokwisha
hifadhiwa, ni vyema ukasoma maelezo yake kuona kama haina vikorombwezo
(additives) vingine.
Ni ukweli ulio wazi kuwa ukitumia bizari iliyobora utapa faida nyingi
kiafya, hivyo hakikisha katika upikaji wako wa kitoweo cha nyama, kama
vile kuku, samaki, ngo’mbe unaweka bizari. Upikaji mzuri ni ule wa
kuweka kiungo hicho mwisho baada ya mboga yako kuchemka na kuiva, kwani
haitakiwi bizari kuchemka sana.
Kwa ujumla hizi ndizo faida utakazozipata ukiifanya bizari kuwa sehemu
ya viungo katika mlo wako wa kila siku:
UTAIMARISHA KINGA YA MWILI WAKO
UTAIMARISHA AFYA YA MACHO
UTAIMARISHA SEHEMU ZA VIUNGIO VYA MWILI WAKO
UTAIMARISHA UTENDAJI KAZI WA INI
UTAIMARISHA CHEMBE HAI ZA MWILI
UTAIMARISHA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA
UTAIMARISHA MFUMO WA DAMU MWILINI
UTASHUSHA KIWANGO CHA KOLESTRO MWILINI
UTAIMARISHA MFUMO WA UZALISHAJI MBEGU ZA UZAZI
UTAIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI MWILINI.
0 Comments