Bamia ni miongoni mwa mboga ambazo baadhi huziona ni za kawaida wanapozitumia kwenye milo yao.

Licha ya kuwa mboga, bamia ina faida nyingi mwilini na kiuchumi. Hulimwa maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo maeneo makavu.  Miongoni mwa faida zake mwilini ni kusaidia kuondosha vimelea vya sumu kwenye ngozi.

Vilevile, inasaidia kuimarisha afya ya nywele na kuongeza kinga ya mwili.  Bamia ina kiasi kikubwa cha Vitamini C, K na folic acid ambayo husaidia mmeng'enyo wa chakula.

Wenye kisukari au majeraha wanashauriwa kula bamia kwa wingi kwani ina mchango katika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu pamoja na kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Ina vitamini A ambayo inasaidia kutengeneza kinga dhidi ya maradhi na sumu ambazo zinaweza zikaingia mwilini.  Mbali na hayo, bamia husaidia kulainisha choo na kuongeza hamu ya kula.

Inasaidia urahisi wa kumeza chakula na huboresha uwezo wa macho kuona.  Kwa wenye uzito uliopitiliza na unene mkubwa, bamia hupunguza lehemu na kusaidia kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Ulaji wa bamia mara kwa mara kwa wanawake husaidia kuponya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi mara kwa mara na hutibu pumu.  Kwa wanaoitumia mara kwa mara, huongeza kinga ya mwili.

Bamia ina wingi wa virutubisho vinavyosaidia kuimarisha afya ya nywele.  Kwa wanaofanya kazi za nguvu au mazoezi mazito, bamia inasaidia kupunguza uchovu wa mwili na msongo wa mawazo.

Bamia inasaidia kusafisha damu, kuponywa mafua, kuondoa sumu mwilini na hutibu vidonda vya tumbo.  Kwa watoto mboga hii ina faida chungu nzima.

Bamia inasaidia kukabiliana na anemia, inazuia utapiamlo huku ikiimarisha mifupa.  Ukiila kwa mpangilio mzuri itakusaidia kuongeza kinga dhidi ya maambukizi ya figo, saratani na pumu.

Kutokana na urahisi wa kilimo chake, kila familia inaweza ikawa na bustani ndogo nyumbani.